Kiswahili

Karibu katika wavuti ya Kiswahili ya mradi wa LHEAf! Hapa unaweza kujifunza mradi wetu unahusu nini na hadi sasa tumefikia wapi.

Lengo hasa la mradi wa LHEAF (Linguistic History of East Africa) ni utafiti wa ukwasi maridhawa uliopo katika historia ya isimu ya lugha za jamii zilizopo katika Afrika ya Mashariki. Mradi huu unafadhiliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kisayansi ya Uholanzi (NWO)  ambayo ipo katika Kituo cha Isimu cha Chuo Kikuu cha Leiden.

Mradi huu unakusudia kurejea historia ya Afrika Mashariki ya miaka 5000 iliyopita hususan nchi za Tanzania na Kenya, kwa kuzingatia utafiti wa isimu, kama tulivyojifunza shuleni kuwa Afrika ya Mashariki mwanzoni ilikaliwa na jamii ya wawindaji na wakusanya matunda na mizizi ambao walikuwa wnazungumza lugha ya Kisani (Khoisan)   Na baadaye jamii ya Kikushitiki ambao ni Wairaqw na Wabantu kama Wasukuma na Wanilotiki kama Wamasai walihamia humo na kuanzisha kilimo, ufugaji na uhunzi.  Tunajua dhana hii ni rahisi mno na ingawa bado kuna maswali kadhaa ambayo bado hayajajibiwa! Mradi huu wa LHEAf unaazimia kuifahamu zaidi historia ya Afrika ya Mashariki.  Kutokana na sababu hii,  baadhi ya lugha ya baadhi ya jamii  kama Kikushitiki na Kibantu zinapaswa kufanyiwa utafiti wa kina.  Hususan maneno yaliyoazimiwa kutoka lugha moja kwenda nyingine pia kuna haja ya kufanyiwa utafiti ili kubainisha jinsi vikundi vilivyokutana katika muda fulani na kuweza kubadilishana lahaja zao.  Mkutano wa mwisho unaokusudiwa kufanyika Juni 2024 utahusianisha matokeo ya utafiti wa  mradi mintaarafu ya   isimu  na utaalamu wa kiakioljia na kinasaba (kijenitiki) ili kutanabahisha yaliyotokea katika Afrika ya Mashariki katika zama hizo.

Beer, S. J., A. Harvey, M. Mous, C. Rapold, T. Schrock, na A. Sosal (kuonekana). Mawasiliano yaliyosababishwa na mabadiliko (RASIMU).

Ikisiri na rasimu

Lugha za Kikushitiki za Kusini za nchini Tanzania katika muundo wake wa sauti zina vizuizi kewa viwili vilivyo sambamba (fricative) and ejective lateral affricate. Sauti zote hizo mbili zinaweza kuonyeshwa na kurithiwa kutoka Kikushitiki na Kiafroashitiki ambayo yanawezesha kuundwa upya kwa matamshi ya kugandamiza hewa (fricative). Hate hivyo lugha za Kikushitiki ya Kusini ndizo lugha za pekee za Kukushitiki zinazodumisha matamshi ya mgandamizo wa midomo. Katika eneo ambalo lugha hizi zipo na zilizungumzwa kuna lugha nyingine ambazo hazihusiani na sauti hizo. Lugha hizo ni Kihadza na Kisandawe.

Kipengele hiki kimependekezwa kama uchunguzi mmoja wa Bonde la Ufa la Tanzania kama eneo la kisimu. Katika hali kama hiyo uwepo wa lateral katika eneo hilo inaweza kufasiriwa kama uhifadhi unaoauniwa na mwasiliani wa sauti tofauti. Ziada vikundi vya lugha katika Afrika Mashariki ambavyo viambajengo vimethibitishwa na Kuliak (Nilo-Saharan) nchini Uganda, yenya lugha tatu na lugha za Kibantu za Wataita nchini Kenya. Katika utafiti huo madhumuni ni kubainisha asili ya sauti (mapokei, mawasiliano au uvumbuzi). Andika hili linafuatilia michakato ay kihistoria katika mawasiliano ya lugha ambayo ilisababisha mgandamizo katika Afrika Mashariki.

Gibson, H. na M. Mous (kuonekana). Ushirikiano wa Kirangi na Kialawa (RASIMU).

Ikisiri na rasimu

Sura hii hii inachunguza matokeo ya uhusiano kati ya jamii inayozungumza lugha za Warangi na Waalawa.  Kirangi ni lugha ya Kibantu inayozungumzwa na watu takriban 310,000 wanaoishi katika eneo la kati ya nchi ya Tanzania.  Kialawa ni lugha ya Kikushitiki inayozungumzwa na watu wapatao 52,000 katika eneo hilo.  Historia za Tanzania ya kati zinaeleza kwamba lugha hizi kwa pamoja zimekuwa zikitumika kwa muda mrefu hadi sasa.  Hapa tunafafanua ushirikiano uliodumu wa kihistoria na mawasiliano miongoni mwa jamii hizi mbili katika kuimarisha uhusiano katika ujamaa na ndoa ambapo kuna ushahidi wa kutosha wa uhusiano unaodumu.  Makala hii inaeleza mazingira ya uhusiano wa kijamii katika utamaduni na matumizi ya Kiswahili kama lugha ya pamoja katika eneo hilo.

Mous, M. na C. Rapold. Kuangalia upya mkopo wa Kikushitiki katika lugha ya Wanilotiki wa Kusini [Hotuba kwenya Rift Valley Network Webinar tarehe 14 June 2023]. DOI: https://doi.org/10.5281/zenodo.8060115.

Ikisiri na video

Makala hii inaangalia uhusiano uliopo katii ya Kikushitiki na Kinilotiki kwa kuanzia hna lugha za Kikushitiki cha Pro Baz.  Proto Baz ni lugha ya Kikushitiki tambuka kwa Wakushitiki wa mashariki kama ilivyopendekezwa na Heine, Rottland na Vossen (1979), kwa kuzingatia maneno yaliyokopeshwa kwa Kinilotiki cha kusini.  Baadhi ya maneno yameshachanganuliwa na Ehret (1970, 1971, 1974). Uchambuzi wa kina wa maneno yaliyokopeshwa unaonyesha kuwa kuna tofauti  kubwa katika asili ya maneno hayo kama ilivyodhaniwa hapo awali.  Hata hivyo, hakuna haja ya kudhania  kuwepo kwa lugha nyingine (Pro Baz) ili kuthibitisha ukopeshaji huo.  Badala yake, mkopo ulitokana na minyambuliko ya lugha za Kikushitiki za sasa. Tujadili uhusiano uliopo hivi sasa katika  lugha za jamii hizo za Wakushitiki wa Mashariki na  Wanilotiki wa Kusini pamoja changamoto zilizopo katika ufafanuzi wa kihistoria kwa kuzingatia ushahidi uliopo.  Kiambata kinampa msomaji muhtasari wa maneno kutoka vyanzo vya mwanzo na mchanganuo unaopendekezwa.

Mous, M. na N. van der Vlugt (kuonekana). Ushawishi wa lugha ya Kikushitiki katika lahaja za wanyama madume (RASIMU).

Ikisiri na rasimu

Kwa asili lahaja za wanyama katika lugha za Kibantu za Afrika ya Mashariki zimetokana na lugha za Kikushitiki.  Mifano iliyo dhahiri ni maneno ya ndama na maziwa katika lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za Kibantu za Afrika ya Mshariki.  Tunakusudia kufuatilia lahaja za mifugo za Afrika ya Mashariki ili kubaini ni lini na wapi lahaja hizo za Kikushitiki za mifugo zimeingia katika lugha za jamii za Kibantu za sasa na pia kuchunguza jinsi zilivyoendelea kuenea za kutoka lugha za Kibantu hadi lugha nyingine kwa kuangalia matokeo mengine kama ni ya kawaida au siyo ya kawaida (kiashiria cha Wabantu kukopa).  Hii ni kufuatilia kukua kwa jamii ya Kibantu katika Afrika ya Mashariki.  Zaidi ni kufahamu mabadiliko ya utamaduni.  Katika makala hii  tuanynaonyesha matokeo ya awali ya lahaja za mifugo dume.  Tunaonyesha lugha za Kibantu za Afrika ya Mashariki  zimeibua lahaja za mifugo dume na chanzo kikubwa ni Wakushitiki wa Kusini kwa sehemu kabla ya jamii hizi za lugha hazijaingi Tanzania hasa upande wa mashariki mwa Ziwa Nyanza, kama sehemu walipokutana, ambapo jamii ya Kibantu ilipofika iliwakuta  wenyeji jamii ya Kikushitiki. Tunaona uibuaji wa lahaja inaashiria uzalishaji wa Wabantu kutokana na ushawishi wa Wakushitiki.

Mous, M. Kutathmini mapendekezo ya mkopo wa maneno ya Kikushitiki na historia yao kwa njamii za Kibantu wa Afrika Mashariki [Hotuba kwenya mktuano Descriptive Linguistic Seminars tarehe 16 February 2024]. Leiden, Uholanzi.

Ikisiri na maonyesho

Ukopeshaji wa awali wa maneno ya jamii ya Kibantu wa Afrika Mashariki unadhaniwa kuwa umetokana na Wakushitiki na hii inaonekana wazi kwa vile Wabantu waliwakuta Wakushitiki katika Afrika ya Mashariki ambapo waliiga maendeleo mbalimbali kama vile kilimo, ufugaji na taratibu nyingine za kijamii. Inasemekana kuwa ukopeshaji huo umeimarisha historia ya isimu na utamaduni katika Afrika ya Mashariki (Ehret 1974, 1998). Kumekuwa na tabia ya kuchukulia ukopeshaji huo kirahisi kama vile umetokana na Kikushitiki. Philippson (2013) anatoa ufafanuzi muhimu mintaarafu ya mapendekezo hayo, hususan yaliyotolewa la Ehret (1998). Andika hili linatoa ufafanuzi zaidi juu ya utafiti wa Philippson, kwa kutumia andiko la Kiessling na Mous (2003), West-Rift Southern Reconstruction. Tunapendekeza maendeleo mapya mintaarafu ya ukopeshaji dhahiri wa Wakushitiki.

Punda, wapumbavu na husiano wao na kiziwi katika Afrika ya Mashariki.